Baba akamatwa akimbaka binti yake huko Mara


Jeshi la polisi wilayani bunda linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumbaka binti yake wa kuzaa ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi
Afisa tarafa ya chamriho, bw. Boniphace maiga, amemtaja mwanaume huyo kuwa ni athuman jeck mkazi wa kijiji cha mariwanda, kata ya hunyari wilayani hapa.
Amesema kuwa mwanaume huyo alimfanyia unyama huo binti yake wakati mke wake akiwa amekwenda kwenye biashara, zake ambapo anadaiwa kumfungia ndani ya nyumba yao na kuanza kumbaka.
Baada ya kitendo hicho binti huyo alikwenda kumwambia mama yake mzazi huku akitokwa na damu sehemu zake za siri
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini