Zoezi la bomoa bomoa lapiga hodi Kahama


Zoezi la bomoa bomoa linaloendelea nchini kwa kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye maeneo ya wazi limeingia wilayani Kahama kwa hatua ya kwanza ambayo itazikumba kata za Kahama Mjini, Majengo, Nyahanga, Nyasubi na Nyihogo.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba ambaye amesema kwa kuanza katika Kata hizo tayari viwanja 48, wamiliki wake amewataka wawasilishe ofisini kwake nyaraka za kumiliki maeneo hayo.

Msumba amesema baada ya zoezi hilo la kuwasilisha nyaraka za umiliki wa maeneo hayo zitachunguzwa upatikanaji wake na hati miliki zitapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana kwa ajili ya kufutwa na baadaye zoezi la kubomoa litaanza kwa maeneo hayo.

Ameagiza umiliki wa maeneo ya hoteli za CDT na zahanati ya Community Health Dispensary uchunguzwe na hatua za ubomoaji ziendelee ikithibitika madai kuwa maeneo hayo ni ya wazi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika Halmashauri hiyo Joachim Henjewele, tayari kikosi chake cha ramani na mpango mji kimeanza uchunguzi kwenye eneo hilo ambalo linadaiwa kuwa ni la wazi ambalo lilikuwa miliki ya vijana kabla halijavamiwa na watuhumiwa hao.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini