Maamuzi Mapya ya Rais MAGUFULI Kuhusu Serikali Kupunguza Matumizi ya Fedha

Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanuzi wa maagizo ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo yalazima katika Wizara, idara na taasisi za serikali. 
Katika ufafanuzi huo Balozi Sefue amemtaka kila mtendaji mkuu ama Afisa Masuhuli wa Serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
“Rais ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vema kila mtendaji mkuu wa Serikali, ajiulize endapo Rais Magufuli atafika katika eneo langu la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake??” amesisitiza Balozi Sefue. 

Kutokana na ufafanuzi huo Balozi Sefue pia amezungumzia uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu yaani “Diaries” akisema kila Mtendaji mkuu wa Serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza na kuchapisha kalenda na Diary? Na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani? 
“Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na Diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha” ameongeza Balozi Sefue. 

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam, Novemba 28, 2015
Na hii hapa chini ndio nakala halisi ya barua toka Ikulu>>
image-28-11-15-14_58

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini