Shambulizi Laua Watatu Kwenye Kliniki ya Wazazi Colorado, Marekani [+PICHAZ]

marekani (1)marekani (2)marekani (3)marekani (4)marekani (5)marekani (6)marekani (7)marekani (8)Shambulizi marekani (1)Mmoja wa waathirika wa tukio shambulio hilo akihojiwa na vyombo vya habari.
Shambulizi marekani (2) Polisi wakiwa kwenye doria.Shambulizi marekani (3)Polisi wakiwa kwenye doria.Shambulizi marekani (4)
Colorado, Marekani
Watu watatu akiwemo askari polisi mmoja wamefariki kwenye tukio la kushambuliwa kwa kumiminiwa risasai kwenye kituo kimoja cha kliniki ya wazazi kiilichopo Mji wa Colorado, Magharibi mwa nchi ya Marekani usiku wa kuamkia leo. 

Katika shambulizi hilo watu wengine tisa wameripotiwa kujeruhiwa, japo hakuna majeruhi walio katika hali mbaya. 
Baada ya tukio hilo kutokea, Jeshi la Polisi wa mjini Colorado walianza kumsaka mtuhumiwa ambaye masaa matano baadaye, yeye mwenyewe alijisalimisha kwenye jeshi hilo wakamtia nguvuni. 

Ofisa wa Polisi aliyefariki ametambuliwa kwa jina la Garrett Swasey (miaka 44) ana mke na watoto wawili. 
Meya wa Mji wa Colorado, John Suthers amesema kuwa, inawezekana shambulio hilo lilipangwa siku chache kabla, na kwamba liliwalenga hasa wakina mama na watoto amabao huwa wanakwenda kwenye kituo hicho cha kliniki kupata matibabu na huduma zingine za kiafya.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini