NDUGAI: Hatuwezi Kumlipa Mtu Ambaye si Mtumishi wa Bunge...

Spika wa Bunge, Mh.Job Ndugai amesema kuwa, Bunge haliwezi kumlipa mtu ambaye sio Mtumishi wa Bunge kutokana na kanuni za Kihasibu.
Amesema hayo wakati alipotafutwa na Gazeti la Nipashe waliotaka ufafanuzi kile ambacho baadhi ya Wabunge kutaka posho zao zielekezwe Jimboni kwao mojamoja badala ya wao kuzipokea ,amesema Mbunge anayetaka hivyo ni vyema akachukua Posho hiyo na kuipeleka Mwenyewe Jimboni kwake.


Pia amedai swala lakufuta Posho ni ligumu kutokana na Kwa sababu za kiusalama Wabunge wanapaswa kukaa katika hoteli zenye hadhi na usalama wakutosha, Hivyo labda kuwepo na uwezekano wakuangalia jinsi ya kuzipunguza.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini