Hii ni Habari Njema Kwa NEYMAR na Mbaya Kwa Cristiano RONALDO




Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kufanya mipango yake mingi na kwa asilimia kubwa kufanikiwa, miongoni mwa ishu alizofanya Cristiano Ronaldo kwa mwaka 2015 ni kuzindua movie ya maisha yake halisi, perfume, viatu vyake lakini hii sio taarifa njema kwake.

football-boots-cristiano-ronaldo-nike-safari-launch

November 27 kutoka El Economista wametangaza kuwa kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike imetangaza kumtaja staa wa FC Barcelona Neymar kuwa ndio staa namba moja kwa sasa anayeuza brand ya bidhaa zao, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa naRonaldo kwa miaka kadhaa ila November 27 Neymar ndio ameandikwa kumzidi Ronaldo.

neymar-promo-nike-reuters

Stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa Neymar kwa mwaka 2016 ndio anatazamiwa kuwa staa atakayefanya vizuri kwa mauzo ya Nike na ndio maana kwa sasa anatajwa kuwa namba moja na Ronaldo kushuka, licha ya kuwa Ronaldo amefanya vizuri kwa miaka kadhaa. Ronaldo na Neymar wote wanamkataba wa kutangaza bidhaa za Nike.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini