Umeipata hii kesi ya TB Joshua mahakamani?


Mchungaji wa Kanisa la Church of All Nations Nigeria, TB Joshua na Wakandarasi wawili ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uzembe uliopelekea jengo la Kanisa hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu 116, leo wameshindwa kufika Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili kuhusu vifo vya watu hao.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu ya Lagos Nigeria baada ya tukio la kuanguka kwa jengo la kufikia wageni lililopo kwenye Kanisa la TB Joshua September 12 2014 na kupelekea vifo hivyo ambapo kati ya waliofariki, 81 walikuwa raia wa Afrika Kusini.
Katika Mashtaka yaliyofunguliwa Mahakamani, Kanisa hilo limedaiwa kufanya ujenzi wa jengo hilo la ghorofa sita bila kuwa na kibali cha kufanya ujenzi huo.
Kwa upande wa TB Joshua wamekuwa wakijitetea kwamba sababu ya jengo hilo kuanguka inatokana na ndege moja ambayo ilizunguka juu ya jengo hilo, muda mfupi baadae jengo hilo likaanguka.. anaamini kuna hujuma zilizofanywa kwenye tukio hilo.
Kukosekana kwa T B Joshua na wakandarasi hao kumelalamikiwa pia kwamba ni kitendo cha makusudi na hakuna sababu yoyote ya msingi, japo mmoja wa wanachama wa Bodi ya kanisa hilo alikuwepo Mahakamani…
Jaji wa Kesi hiyo pia ameonekana kukerwa na kitendo hicho huku akisisitiza kwamba hatovumilia uzembe wa aina yoyote utakaofanya kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka December 11 2015 ambapo TB Joshua na wakandarasi wake wawili wanatakiwa kuripoti Mahakamani hapo, Lagos Nigeria.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini