Kauli ya kwanza ya Sheikh Ponda baada ya kuachiwa huru na mahakama


Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro imemwachia huru kiongozi wa taasisi na jumuiya za kiislam nchini sheikh ponda issa ponda baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.


Sheikh ponda ameachiwa huru na Hakimu mkazi mfawidhi Mary Moyo baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na kile kilichoelezwa kuwa dhamana yake ilizuiwa na mkurugenzi wa mashtaka DPP kwa maslahi ya taifa. 


Akizungumza mara baada ya kuachiwa huru sheikh Ponda amesema kuwa anaishukuru mahakama kwa kutenda haki japo kuwa imechelewa na kwamba amekaa rumande tangu siku aliyokamatwa kutokana na dhamana yake kuzuiwa. 


Katika kesi hiyo iliyovuta watu wengi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu sheikh ponda alikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo alidaiwa kuyatenda agosti 10 mwaka 2013 katika viwanja vya shule ya msingi k.ndege manispaa ya morogoro. 


Upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Bernard Kongola, Sunday Hyera, na George Mbalassa wakati upande wa utetezi uliongozwa na wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na Batheromeo Tarimo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini