Kama Real Madrid watamuuza Cristiano Ronaldo, unajua Rafael Benitez atasemaje?

Headlines nyingine za soka kutoka Hispania zinazo muhusu staa wa soka wa Urenoanayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo na kocha wa klabu yake Rafael Benitez zimenifikia November 29, kuhusu wawili hao ambao wamekuwa wakihusishwa kutokuwa na mahusiano mazuri kwa siku za karibuni na sababu zimekuwa zikitajwa tofauti tofauti. 

Stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk zinataja kuwa kocha wa klabu ya Real Madrid yaHispania Rafael Benitez hatolalamika wala kuchangia chochote kama Real Madridwataamua kumuuza Ronaldo, hizi ni stori za uchunguzi ambazo pia zinadhiirisha kuwa wawili hao hawapo vizuri kwani kwa nyota kama Ronaldo kuondoka katika klabu fulani na kocha wake akubali kirahisi huwa ni ngumu sana.
Shakhtar-Donetsk-vs-Real-Madrid
Benitez anaelewa kuwa Rais wa Real Madrid Florentino Perez yupo katika presha ya kifedha ya uchaguzi wa kutaka kuwania awamu nyingine, hivyo lolote linaweza kutokea,Ronaldo amekuwa akihusishwa kwa siku za hivi karibuni kuwa na mpango wa kurudi Man United au kutimkia klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini