Wachimbaji 4 wamefariki dunia na 1 bado hajapatikana kwa kufukiwa na kifusi Geita


Watu wanne wamefariki dunia na mmoja bado hajapatikana kwa kufukiwa na kifusi katika eneo la Prospect 30 lililopo eneo la mgusu wilayani Geita.


Wakizungumza nasi baadhi ya wachimbaji hao wamesema hali duni ya maisha huwalazimu kufanya shughuli hiyo hatarishi bila kuzingatia usalama ambapo wameiomba serikali kusaidia kundi la wachimbaji wasio rasmi ili wapate eneo la kuchimba kwa usalama.

Manase Ndoroma ni meneja mahusiano ya jamii wa mgodi wa dhahabu wa Geita amewataka vijana wanaojishughulisha na uchimbaji kuzingatia usalama wa miamba wanayotafuta dhahabu hasa msimu huu wa masika kutokana na eneo lenyewe kuwa na mwamba laini.

Aidha kaimu afisa madini mkazi mkoa wa Geita Fabian Lucas amesema eneo hilo linamilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya mgodi wa dhahabu wa Geita na kwamba wachimbaji hao wasiorasmi wameingia kuchimba eneo hilo kinyume na sheria hivyo kuwataka kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa maeneo na leseni kihalali.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini