Wabunge Imekula Kwao...Bunge Limekataa Kuongeza Dau Kwenye Hela ya Kununua Magari 'Mashangingi'


Msemaji wa Bunge amesema kuwa hawajapata malalamiko rasmi kutoka kwa wabunge kuwa wanahitaji kuongezea fedha hizo zifikie milioni 130 kutokana na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani. 

Mbunge Ezekiel Maige amesema kuwa afadhali Serikali iwanunulie magari kabisa kuliko kuwapa fedha
Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Abdallah Mtolea amesema wapewe fedha wakanunue wenyewe, pia amedai kuwa bei ya gari Land Cruiser(Mkonge) ambayo wabunge wanatakiwa kununua gharama yake sokoni ni milioni 130
Awali baadhi ya wabunge walidai kuwa wapewe milioni 130 kutokana na kupanda kwa bei ya magari wanayotakiwa kununua.
Wabunge wa Bunge la 10 walipewa milioni 90 za kununua gari.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini