Miaka Mitatu Tangu SHARO Milionea Afariki Kwa Ajali ya Gari..(+VIDEO)


November 26 2015 ni siku ya kumbukumbu ya Sharo Milionea ambae ametimiza miaka mitatu toka afariki dunia kwenye ajali ya gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR alilokua akiliendesha mwenyewe kutoka Dar es salaam kwenda kwao kijijini Lusanga wilaya ya Muhenza Tanga.
Kama umemis taarifa kuhusu kumbukumbu yake unaweza kutazama post iliyopita.

Wakati huu ambapo msanii na mwigizaji marehemu Sharo Milionea anatimiza miaka mitatu toka afariki, mmoja wa marafiki zake ambae ni mchekeshaji/Mwigizaji Kitale kupitia instagram alipost picha ya Sharo na kuandika…’Leo ni tarehe 26/11/2015 na marehemu alifariki 26/11/2012 tarehe kama ya leo ni Miaka 3 sasa tokea Afariki Marehemu Hussein Ramadhani Mkiety kwa ajali ya gari Mkoani “TANGA” Eneo la “MAGUZONI” wilaya ya “MUHEZA” msiba ulikuwa kijijini kwao LUSANGA Na tulimzika kijijini kwao hapohapo LUSANGA anapoishi mama yake mzazi R.I.P Sharo Milionea……….Naomba Tumuenzi Kwa Pamoja Leo ndugu yetu MBELE YAKE NYUMA YETU’ – mkudesimbaoriginal

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini