SAD NEWS: MAMA AFARIKI BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WATATU HUKO MISUNGWI..SOMA ZAIDI HAPA!
‘Ni kweli tumepokea Watoto watatu ambao ni wachanga wakiwa na kilo 1.7 na 1.8 kutokea Misungwi, mama yao alifariki muda mfupi tu baada ya kuj i fungua na chanzo ni maamuzi yake ya kukataa kupewa matibabu yanayohitajika ambayo ni kufanyiwa Opareshen’ ‘Aliweka saini kabisa ya kukataa kufanyiwa opareshen ili ajifungue kwa kutumia njia hiyo hivyo ikabidi ajifungue kwa njia ya kawaida ambayo ilimfanya atokwe na damu nyingi sana na ndicho kilichosababisha kifo chake’ h i zi ni sentensi za mwanzo kutoka kwa Dr. Baraka Malegesi wa hospitali ya Bugando ambao ndio imewahifadhi hawa watoto kwa sasa. Akihojiwa na Millard, Dr. Malegesi ameendelea kusema ‘tumewapokea watoto na bado tuko nao hapa tunawahudumia vizuri wako na mama yao mdogo lak i ni hali ni ngumu kwa sababu maisha ni magumu kwake na tumejitolea hospitali kuwapa maziwa lakini gharama ni kubwa kwa sababu wiki ni zaidi ya elfu 70 kuwahudumia sasa katika kipato cha chini ndugu zak...