SOMA MANENO YENYE UCHUNGU MWINGI NDANI YAKE YALIYOSEMWA BAADA YA KIFO CHA JANA CHA BETTY KUHUSU MITANDAO!!



"Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya askari JKT,JWTZ au hata Polisi kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza.


Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, Facebook na Instagram lakini ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah! huyu ana matusi si mchezo!'


Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo.


Marehemu Betty ni victim wa yote hayo. Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria, superstar uchwara n.k.. na ninaamini hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa."

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini