BAADA YA KUPIGWA RISASI: PRODYUZA SUGE KNIGHT ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Prodyuza Suge Knight wakati akiwasili katika klabu ya usiku ya 1Oak ambapo baadaye alishambuliwa kwa kupigwa risasi sita.

PRODYUZA Suge Knight ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Cedars-Sinai, Los Angeles nchini Marekani alipokuwa amelazwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi katika klabu ya usiku ya 1Oak kwenye pati ya utangulizi wa utoaji Tuzo za VMA Jumamosi usiku.


Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akipatiwa huduma ya kwanza.
Suge aliruhusiwa jana na ataendelea na matibabu madogomadogo akiwa nyumbani kwake.

Mbali na kujeruhiwa, Suge anadaiwa kutotoa ushirikiano kwa polisi kuhusu tukio hilo lililotokea katika pati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki Cris Brown anayedaiwa kuwa ndiye alikuwa mlengwa mkuu wa shambulio hilo.


Mwanamitindo Megan Hawkins akiwa hospitali ya Cedars-Sinai baada ya kujeruhiwa kwenye shambulio hilo.
Suge alipigwa risasi sita, nne tumboni, moja kifuani na nyingine mkononi ambapo watu wengine wawili akiwemo mwanamitindo Megan Hawkins nao walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Cedars-Sinai kwa matibabu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini