KIMENUKA MBAYA: AUNT ACHEFULIWA NA DIVA WA CLOUDS..KISA KUMCHAFUA INSTAGRAM!

JAMBO limezua jambo! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’ kwa madai kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Peter ‘Moze Iyobo’, jambo ambalo ni uongo.
Prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’
Akizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu, Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji kumchafua akimsingizia kuwa ni mjamzito, jambo ambalo limemsababishia matatizo kwenye ndoa yake na mumewe Sunday Demonte.

“Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina mimba ya Moze Iyobo, imeniuma sana.
“Hebu vuta picha wakwe, mawifi na mashemeji ambao tayari wameshasikia na kusoma kwenye ukurasa wa Diva, akisema mimi nina mimba ya yule mtoto, dah! Nimeumia sana, kwa kweli siwezi kuliacha lipite hivihivi.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson
“Huyo Diva lazima nitasimama naye mahakamani,” alisema Aunt.
Hivi karibuni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diva aliandika: “Wakati sakata la mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze Iyobo likipamba moto, mimba ambayo ni tangu Mwezi wa Ramadhan, sasa hesabuni miezi, hapa ni miezi miwili au mitatu.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini