HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI HADHARANI BAADA YA KUKABIDHIWA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI!

\\

Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu.


Wanawake zaidi ya 30 kutoka Kinondoni, Kawe, Pwani na Ubungo jana saa 5.20 asubuhi, walifika katika ofisi za Bawacha jijini Dar es Salaam kumchukulia fomu Mdee wanayedai kuwa ndiye anayestahiki kuliongoza baraza hilo kutokana na msimamo wake wa uongozi wa kutotaka kuyumbishwa.
“Tumekaa na kutafakari ili kumpata mwanamke atakayeweza kuliongoza baraza hili kwa kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi, tumeona Halima Mdee anatufaa zaidi ndiyo maana tumeamua kuja kumchukulia fomu,” alisema Felister Njau, Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kawe.


Huku akishangiliwa na wenzake alisema, “Tunakwenda kumtafuta sehemu yoyote alipo ili tukamkabidhi hii fomu na tutamwomba akubali ombi letu.”


Msafara wa wanawake hao wakiwa na fomu yao mkononi ukiongozwa na Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Kunduchi, Elefedina Mali ulikwenda makao makuu ya chama hicho ambako walimkuta Mdee na kumkabidhi fomu hiyo.
Aliwashukuru na kuwaomba wamvumilie kwani anahitaji muda wa kulitafakari ombi hilo.
Huku akibubujikwa na machozi, Mdee (pichani) alisema; “Nimewaelewa naombeni nikajitafakari kwanza, nitawaeleza nitakachoamua.” Wanawake hao pia walichangishana fedha Sh53,000 walizomkabidhi Mdee kwa ajili ya kurejeshea fomu hiyo.
You migh

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini