DUH...KUMBE MARAFIKI WA BONGO MOVIES NDIO WAPO HIVI!!

Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford.
STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa hana rafiki yeyote maarufu ndani ya Bongo Movies. 

Akizungumza na paparazi wetu, Shamsa alisema kuwa tangu huko nyuma alishawafuta marafiki wote ambao ni wasaliti na badala yake mtu pekee ambaye ni rafiki yake ni mwigizaji mwenzake, Wellu Sengo ambaye anachipukia. 

“Unajua ni bora uwe hata na rafiki mmoja ambaye anakujali na kukuthamini, wengine wote mimi niliwafutilia mbali kwa sababu ukiwa nao wengi wanaweza kukutia hata ‘stress’ zisizokuwa na maana kabisa,” alisema Shamsa.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini