HABARI YA KUTISHA UKATILI WA AJABU SANA KWA MIFUGO MOROGORO!!

Ng’ombe zaidi ya 80 wameuawa kikatili kwa kukatwakatwa na wengine kuchinjwa baada ya mifugo kuingia katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Kisara na Mbogo wilaya Mvomero mkoa wa Morogoro .
 
ITV imeshuhudia mabaki ya nyama na ngozi za na ndama wachanga  waliondolewa katika matumbo ya ngombe waliochinjwa  na kisha nyama  kuuzwa katika mabucha huku ngombe wengine wakiwa wamekatwa miguu na kushindwa kutembea ambapo wamiliki wa ngombe hizo ambao ni wafugaji  wamelalamikia wakulima kuchukua hatua mkononi na kuomba serikali kuchukua hatua.
 
Nao baadhi ya wakulima wa wilayani Mvomero walioshuhudia tukio hilo wameonyesha kusikitishwa na tukio hilo huku wakiitaka serikali kuhakikisha inapanga mipango mizuri ili kunusuru migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kutenga maeneo maalumu kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
 
Nae mkuu wa wilaya ya Mvomero Antony Mtaka akizungumzia tukio hilo amesema serikali ya wilaya imeanza kuchukua hatua kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili waliohusika na tukio hilo wachukuliwe hatua za kisheria huku akiwataka wafugaji kutulia wasilipize kisasi.
ITV

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini