DUNIA IMEKWISHA: DENTI WA CHUO AMUUA MWANAYE, AMFICHA UVUNGUNI!

MWANAFUNZI wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya,  Vena Mtati (27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya kitanda!
Vena Mtati akitahayari baada ya kutiwa mbaloni na polisi.
Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi, lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya Mvinjeni mjini hapa. 

SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito. 

“Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho. 

Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.
“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.

Akiwa chini ya ulinzi.
“Tuliposikiliza kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili kufanya kelele hizo zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani  tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),” kilisema chanzo hicho. 

HATUA ZA HARAKA
Mwandishi wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.
Polisi hao, awali walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce ambaye alikuwa kwenye  mihangaiko yake.

 Alipopatikana alipokonywa simu yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.
Aliulizwa kama ana mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama mgeni huyo amejifungua, akakataa ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani kwake kumfuata mtuhumiwa huyo. 

ASKARI WAFIKA ENEO LA TUKIO
Paparazi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa kama amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada ya  kubanwa na kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri kujifungua na kusema kwamba mtoto huyo amemficha uvunguni mwa kitanda.

Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
DAMU SAKAFUNI
Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu  zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe! 


POLISI WAPEKUA UVUNGUNI
Polisi walizama chumbani, wakainama kuchungulia chini ya kitanda. Walichoanza kukiona ni mfuko wa salfeti, wakauvuta  kuutoa. Walipofungua ndani, wakakuta mfuko wa rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa kimeviringishwa nguo nyingi na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa. 
HEBU SOMA HII, INAUMA ZAIDI
Mbali na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo usitoe harufu utakapotupwa porini. 
Majirani walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa sababu tayari anajua namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye na ujuzi asingeweza kufanya hivyo.

Vena Mtati akiwa na kiroba hicho.
SABABU YA MTOTO KUUAWA
Kuna madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini. 


ORODHA YA WALIOKAMATWA
Baada ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye, mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mara moja. 

Polisi walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu alikiuka sheria za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo kwenye serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa kutambua kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini