Kondom za MALAYA wa Morogoro zawaathiri watoto
Biashara ya ngono iliyokithiri katika mji wa Morogoro imegeuka kuwa kero kwa wakaazi wa eneo hilo na familia zao hali inayowaweka hatarini zaidi watoto wadogo wasio na hatia wanaokutana na kondom zilizotumika huku mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Joel Bendera akinawa mikono kuhusu suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea Morogoro, serikali kuu imekuwa ikitafuta dawa kali ya kuweza kudhibiti biashara hiyo hapa nchini.
Edson
Mkisi Jr wa Times Fm, hivi karibuni alitembelea mkoa huo na kushuhudia
kushamili kwa biashara ya ngono sehemu mbalimbali za mkoa wa Morogoro
hususani katika maeneo ya Kaumba na Itigi mkoani humo.
Taarifa
zilizopatikana awali toka kwa baadhi ya wakazi wa maeneo ya mji wa
Morogoro zilidai kuwa biashara ya ngono imekuwa kero mkoani humo
kutokana na utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika katika mitaa hiyo.
Kondom hizo zilizotumika zinahatarisha afya ya watoto wanaozitumia kama mapulizo.
“Kiukweli
hii biashara mbali ya kutuaibisha sisi akina mama lakini pia inatukera
sana kutokana na utupwaji hovyo wa kondom unaofanywa na hao akina
dada….na baada ya kondom hizo kutupwa watoto wetu wanaziokota na kuanza
kupuliza kama maputo kwakweli inatukera sio siri,” anasema mama Sakina mfanyabiashara maarufu wa samaki Msamvu Morogoro.
Baadae
mwendesha bodabodo eneo hilo alimuonysha mwandishi wetu Hotel moja
maaufu na kudai kwamba Hotel hiyo imekodiwa na MALAYA hao kwa ajili ya
kufanyabiashara hiyo na serikali ya mkoa wanatambua ‘ishu’ hiyo!
“Yaani
hawa akina dada wakiwa ndani ya hiyo Hoteli hakuna mtu anayeweza
kuwakamata ila wakifanya biashara yao nje ndio wanakamatwa na polisi kwa
huku Morogoro maarufu kama Voda Fasta,” anasema dereva bodaboda huyo.
Kutokana
na malalamiko mengi toka kwa wakazi wa Morogoro kuhusiana na uwepo wa
MALAYA hao katika viunga mbalimbali vya mkoa hao, Edson Mkisi Jr,
mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu cha times fm, aliamua kuwasiliana
na Mkuu wa mkoa huo, Bw. Joel Bendara kwa ajili ya kujua serikali ya
mkoa inafanya jitihada gani katika kupunguza ama kumaliza kabisa kero ya
MAKAHABA hao.
Mkuu
huyo wa mkoa alidai kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo la MAKAHABA
wala utupwaji hovyo wa kondom kwa maelezo kwamba suala hilo lina hadhi
ndogo sana ukilinganisha na cheo chake!
“Jamani
hilo suala ni dogo sana kulingumzia mtu kama mkuu wa mkoa….naomba
ufuate protoko mimi siwezi kuzungumzia kondom ukilinganisha na hadhi
yangu hilo suala linamuhusu Mkuu wa Wilaya (DC), Meya ama Diwani sio
mimi jamani,” alisema Bw. Bendera.