PART 2 YA TEGO LA NGONO LA MFANYABIASHARA MAARUFU KARIAKOO. AKIMBIA MJI KWA AIBU HAJULIKANI ALIPO HADI SASA NYUMBANI HAYUPO DUKANI HAYUPO MKEWE ANALIA MASAA YOE..!



Na Mwandishi Wetu
Gazeti hili toleo namba 21 la Jumatano wiki iliyopita liliwaletea habari iliyokuwa inasimeka MAFANYABIASHARA MAARUFU KARIKOO ANASAKA TEGO LA NGONO na kuwaeleza wasomaji wetu kuwa hitimisha la taarifa hiyo ni lazima mtuhumiwa Daud John Mpenda apatikane ili kuelezea kwa nini amekuwa akijihusha na matukio ya udhalilishaji kwa wanawake za watu na mabinti wadogo.
Timu yetu ile ile iliyofanikisha zoezi la kumnasa mfanyabishara huyo ndiyo iliyoingia mtaani tena kumsaka kwa ajili ya kupata kauli yake lakini katika hali isiyotarajia toka Jumatano siku gazeti lilipotoka wiki iliyopita Bw Daud amekimbia mji kabisa ofisini kwake hapatikani wala nyumbani huku kukiwa na taarifa kuwa amepotea kabisa na hajulikani alipo huku wengine wakisema labda amekimbilia nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Daud ambae anaishi nae jirani maeneo ya Mbezi Beach aliliambia Maskani Bongo kuwa" Jamani tangu gazeti lenu lilipoanika picha za tukio  lake jamaa kahama mji na hata mkewe hajui amahara alipo hali inayotia hofu kuwa huenda atakuwa ameenda mbali" Alisema mwanamke huyo
Mapaparazi wetu waliweka kambi jirani na duka lake na Mpenda Mibile Phone  lilipo mtaa wa Uhuru Kariakoo kwenye kona ya mtaa wa Agray kwa siku tatu kwa ajili ya kuona kama ataonekana ofisini lakini wapi hakupatikana ng'oo.
Hata hivyo dodosa za mapaparazi wetu kwa majirani wa Daud hapo Karikaoo bila nao kufahamu kama wanaongea na mwandishi wetu walitoa habari mpya kuwa tangu habari hiyo itoke mtaa mzima Agray umeshtushwa kwani inadaiwa kuwa kuna shemeji yake ambae amemuweka dukani hapo huwa anamlamba kwa siri hivyo baada ya habari hiyo basi nae alitimka hadi leo hajaonekana.
Mapaparazi waifanyajitahada za kupata namba za simu na shemejie huyo aliyetajwa kwa jina moja la Diana na mkewe halisi Daud aliyefahamika kwa jina la  Gati Juma ambae ana mtoto mdogo na bado anamnyonyesha na Diana ndiye aliyekuwa wa kwanza kipigiwa simu lakini hakupokea kabisa licha ya kutumiwa na ujumbe wa meseji kama anaombwa apokee lakini wapi.
Upande wa mkewe nae alipopigiwa simu na nae pia hakuweza kupokea na kulikuwa na taarifa kuwa familia ya Daud ilikuwa na kikao kikubwa cha kumfariji mkewe huyo kutokana na tukio hilo huku wakimsihi asichukue maamuzi yoyote awe na subira kwanza hadi atakapopatikana Daud ili aje kutoa maelezo juu ya tukio hilo.
Katika hatua nyingine baada ya kupatwa na msara huo marafiki wote wa Daud aliokuwa anakunywa na kula nao waliingia mitini" Nakwambia marafiki watu wabaya sana baada ya tukio la Daud marafiki zake wote wameingia mitini hata yuko Maliki ambae ni kuhadi wake anaempatia mademu nae amekimbia na kumcheka hii ni hatari sana" Alisema jirani huyo Karikoo

Hata hivyo kabla ya gazeti hili kuingia mitamboni kulikuwa na taarifa toka kituo cha Polisi Oysterbay kuwa mfanyabishara huyo anatakiwa kulipoti kutuoni hapo kwa ajili ya kuhojiwa upya kwa kitendo chake cha kutoa taarifa za uwongo kwa  Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni" Hili ni kosa kutoa taarifa za uwongo ndani ya Jeshi la Polisi hivyo ni lazima tutachukua hatua za kisheria juu yake hivyo tunamtaka afike hapa mara moja licha ya kwamba simu zake hazipatikani lakini akipata ujumbe huu atekeleze agizo hilo" Alisema mmoja wa wapelelezi wa tukio hilo ambae aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa yeye si msemaji wa Jeshi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini