SHOCKING: MTOTO WA MIAKA 9 ALIVYOMUUA MWALIMU WAKE

Hii ni sehemu ya video ya mfunzo hayo kabla ya tukio.
Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliyekua anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun iliyotengenezwa Israel.


Mtoto huyu wa kike anaetokea New York alikua kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukua time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambae alifariki baadae hospitalini.
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikua na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu.

Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini