ATESEKA KITANDANI MIAKA MITATU
Johanitha Robert Mulokozi amekaa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.
INASIKITISHA! Johanitha Robert Mulokozi (31) amekuwa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.Mama huyo mwenye mtoto mmoja amekuwa akisumbuka na ugonjwa huo uliomfanya akose raha licha ya kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akisimulia
huku akilengwalengwa machozi Valentina alisema: “ Tatizo la mwanangu la
kupooza mwili mzima lilianzia pale alipodondoka chini baada ya kupata
taarifa za kifo cha baba yake mwaka 2011.
“Sikutegemea kama mwanangu angekuwa
hivi kwani alikuwa akiishi vizuri na alikuwa akiendelea na maisha yake
hasa baada ya kupata mtoto ambaye anamtegemea.
“Baada ya kupata tatizo hili
nilimpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na alilazwa pale kwa
matibabu lakini hali bado ikawa mbaya.
“Ninachoweza kusema mimi ni kwamba
sikukata tamaa, niliendelea kufanya juhudi kuokoa maisha yake licha ya
kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa muda wa miezi sita pasipo
kupata nafuu na kuamua kumrudisha nyumbani.
“Baadaye nilipata wazo la kumpeleka
katika Hospitali ya Regence jijini Dar na nilipofika pale na kuwaelezea
tatizo la mwanangu, walimpima na madaktari walibaini kuwa tatizo lake
linaweza kutibika nchini India, nikaambiwa nitafute shilingi milioni
kumi na tatu. Nilishika kichwa na kuanza kulia.
“Nililia kwa sababu nilijiuliza,
nitapata wapi fedha hizo niokoe maisha ya mwanangu. Niliamua kumfuata
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa na kumuelezea tatizo langu.
“Namshukuru sana baba yule (Jerry)
kwani baada ya kumpa maelezo na kumuonesha barua ya safari ya India
aliingiwa na huruma , akaniandikia hundi ya shilingi milioni sita
(6,000,000/), hivyo nina upungufu wa shilingi milioni saba ili mwanangu
aweze kupelekwa India kwa matibabu,” alisema mama huyo huku akifuta
machozi kwa kanga yake.
Mgonjwa hakuweza kuzungumza na gazeti hili na badala yake wakati wote wa mahojiano na mama yake alikuwa akilia wakati wote.
Yeyote aliyeguswa na tatizo la mama
huyu na angependa kumsaidia mchango anaweza kuwasiliana naye kwa namba
ya simu, 0714599104, 0754086888. KIROHO SAFI TU