Hawa walisherekea kifo cha Mwalimu Nyerere, leo wanamtumia kuutaka urais!



Tuachane na Josephat Gwajima anayejiita ni mchungaji japo sijui nani alimtunuku uchungaji na kwavigezo vipi, yeye hana tofauti na sigara kali

Aliyekuwa anaamini Kingunge ni kiongozi wa kitaifa atafakari upya,Jiulizeni kwa nini hakupata nafasi ya juu kama Mzee Kawawa enzi ya mwalimu?

Ni Kingunge huyuhuyu alifukuzwa ukuu wa mkoa singida na Mwalimu Nyerere, leo anajivika chanda cha Mwalimu.

Lowa alifukuzwa uanachama wa TANU kwakosa la kuiba pesa ya ujenzi wa ofisi za umoja wa vijana wa Tanu jijini Arusha yeye akiwa ni katibu wa vijana mkoa,

Ni Moringe na baadhi ya wazee waliopiga magoti kumuombea punguzo la adhabu na hivyo akapewa adhabu ya kuwepo Lumumba tu bila kazi yoyote kwa mda wa mwaka mzima.

Katibu wa vijana TANU Taifa ndugu Elly Anangisye alifukuzwa moja kwa moja na ubunge wa Rungwe akavuliwa.

Alipofariki tu Mzee Nyeree, Lowasa na kundi lake walifanya party na kupongezana, wengine walipigiana simu hata kabla hajafa kuwa kikwazo kimeondoka,

Leo kutangaza nia ya urais wanamtaja Mwalimu kama mbeleko.

Rip J.K Nyerere

BY Yericko Nyerere/JF

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini