Haya ni maajabu ya pete ya kuokota yanayomtokea huyu !


ring_sakawa 
Kijana mmoja kutoka Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeanza kupuputika huku nyama za kidole hicho zikionekana kulika.
Kijana huyo Eric Buageng, alisema iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole chake, akaanza kusikia maumivu na pete hiyo ikaanza kumbana kidole.
Eric-Buabeng
Eric Buageng
Eric amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa ukitetemeka, akashindwa kuitupa pia, halafu akasikia sauti ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anasikia sauti ikimwambia atoke nje.
Jitihada zake zimeonekana kutokuwa na matumaini yoyote kwenye mikasa inayomkuta kwenye pete hiyo, ameshaenda Hospitali  na pia kwa wachungaji na hakuna mafanikio yoyote huku wakihisi kwamba pete hiyo ina uhusiano na masuala ya uchawi.
files

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini