Ndikumana: Sijaachana na Irine Uwoya Ingawa Hatuishi Pamoja


Mume wa Staa wa filamu za Kibongo,Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Katauti’amesema kuwa hajaachana na msanii huyo kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.

Ndukumana ambaye ni mwanasoka kwenye klabu moja ya soka nchini Rwanda ameyazungumza hayo hivi karibuni wakati alipofanya mahojiano na mtangazaji wa Clouds TV,Zamaradi Mketema alisema kuwa ingawa hawaishi pamoja na Irene Uwoya lakini hawajaachana.

Sijaachana na Irene Uwoya ingawa hatuishi pamoja yeye anaishi Dar mie naishi Rwanda na bado nacheza soka ila nategemea kusomea ukocha baada ya kustaafu soka,’alisema Ndikumana.

Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2008 na kubahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Krish.

Cloudsfm.com

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini