HUWEZI AMINI! Mama Huyu Amla Mtoto Wake Mwenyewe!

indiaaaa


Kumekuwepo na matukio ya baadhi ya wazazi kuwanyanyasa na hata wengine kuripotiwa kuwaua watoto wao wa kuwazaa wenyewe kutokana na sababu mbalimbali.

Headlines nyingine leo zinatokea kule India ambapo mama mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya kuripotiwa kumla mtoto wake wa miaka minne huku akiwa  hai. 

Pramila Mondal ambaye anadaiwa  kuwa na matatizo ya akili alifanya kitendo hicho akiwa nyumbani kwake na kukutwa na shemeji yake akiendelea kumla mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto wake huyo ambaye alikuwa wa kike. 

Baada ya Polisi kufika na kumshilika mama huyo, mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya Malda Medical center huku akiwekwa katika chumba cha uangalizi maalum kutokana na kuwa na majeraha makubwa. 

Polisi walisema pamoja na mama huyo kudaiwa kuwa na matatizo ya akili pia pombe pamoja na madawa vimechangia yeye kufanya tukio hilo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini