Ni kweli Tanzania hakuna Petroli? Ninayo majibu ya Waziri kwenye sentensi zake 7 Bungeni… (Audio)

IMG_1219

Hii sio mara ya kwanza ishu ya kukosekana kwa mafuta inachukua headlines Bungeni, stori zimeenea kwenye mitandao ya Kijamii kuhusu mafuta kutopatikana kwenye Sheli za Mafuta. 

Imefika kwenye Kikao cha Bunge Dodoma leo June 29 2015 na ilianza kumfikia Naibu Spika wa Bunge>>> “Kuna maneno yanasambaa kwenye Mitandao ya Kijamii na mahali kwingine kwamba siku tatu zijazo kutakuwa hakuna mafuta katika Nchi hii, ntaomba uongezee ufafanuzi kidogo wa hali hii” >>> Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai. 

“Haiwezi kutokea na haya si maneno ya kufurahisha.. Tunajua kwa takwimu katika hifadhi za Dar es Salaam kuna mafuta ya kutosha. Sheria na Kanuni zinampa Mamlaka Waziri kuruhusu mafuta yauzwe, nawataka wenye vituo mruhusu mafuta yauzwe asitokee mtu yoyote akaufanya huu uvumi ukawa ukweli. Tunafuatilia mwanzo wa message hiyo.. mimi ni mtaalam wa kupima matenki… mtu yoyote asiingie kwenye mtego huu, kituo kitafungiwa na hifadhi zitafungiwa… leseni ni mali ya Waziri tunaweza kuchukua leseni wakati wowote“>>> Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage.
Hivyo stori  ninayo kwenye hii sauti hapa....

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini