JEURI YA PESA: Floyd Mayweather kununua gari ya dola milioni 4.8, zipo tatu tu duniani!

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather anatarajia kuongeza orodha ya magari ya kifahari anayomiliki kwa kununua ndinga yenye thamani ya dola milioni 4.8.

2A18453B00000578-3143501-image-a-19_1435607633262
Koenigsegg CCXR Trevita ina thamani ya dola milioni 4.8 na zipo tatu tu duniani
Floyd ataumwaga mkwanja huo kununua gari aina ya Koenigsegg CCXR Trevita, ambazo zipo tatu tu duniani.
Ataiongeza gari hiyo kwenye magari yake yenye thamani ya dola milioni 55 yakiwemo Ferrari, Porsche, Lamborghini, Bugatti na ndege binafsi yenye thamani ya dola milioni 30.

Mwaka huu bondia huyo ameshika nafasi ya kwanza ya mwanamichezo aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa kutengeneza mkwanja wa dola milioni 300.
Fedha hizo aliingiza May 2 baada ya kuzichapa na Manny Pacquiao.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini