WANANUKA FEDHA! Wafahamu Wamiliki 11 wa Klabu Matajiri Zaidi Duniani!

LONDON, ENGLAND - OCTOBER 04:  Businessman and Chelsea Football Club owner Roman Abramovich (C) arrives at The High Court on October 4, 2011 in London, England. Russian businessman Boris Berezovsky is alleging a breach of contract over business deals with Mr Abramovich and is claiming more than £3.2bn in damages.  (Photo by Peter Macdiarmid/Getty Images)

 Wamiliki 11 wa klabu matajiri zaidi duniani
 LONDON, England
 KAMA ungeuliza swali la nani anataka kuwa bilionea, kila mtu duniani angenyoosha mkono, lakini haiwezekani duniani wote watu wawe mabilionea, kuna wachache wenye nazo na wengi ambao hawana.
 Katika ulimwengu wa soka, pamoja na Real Madrid kuonekana imejaza wachezaji wa bei mbaya lakini mmiliki wake hayumo kwenye orodha ya wamiliki wa soka matajiri zaidi duniani. Timu inaweza kuwa na hela lakini mmiliki wake akawa na fedha ya kawaida.

Carlos_Slim_Helú 
Carlos Slim Helu (Mexico).
 Unataka kuwajua wamiliki wa klabu za soka matajiri zaidi duniani? Kwa kutumia takwimu za mtandao maarufu wa Forbes, hawa ndiyo wamiliki wa klabu wenye fedha za kutisha zaidi duniani mwaka 2015: 

Carlos Slim Helu (Mexico)
 Utajiri: dola bil 73 (trilioni 159.5)
 Klabu: Pachuca, Leon (Mexico) na Real Oviedo (Hispania)
 Huyu ni tajiri namba mbili duniani. Utajiri wake unatokana na Kampuni ya Telecom anayoimiliki, ambayo inahusiana na mambo ya mawasiliano kwa njia ya simu.

SHEIKH MANSPOUR 
Sheikh Mansour.
 Amancio Ortega (Hispania)
 Utajiri: Dola bil 57 (tri 124.5)
 Klabu: Deportivo La Coruna (Hispania)
 Huyu ndiye Mhispaniola tajiri zaidi, akiwa anakamata nafasi ya tatu duniani. Anakamata mkwanja kutokana na kumiliki Kampuni ya Inditex inayobuni, kuzalisha na kusambaza kila aina ya nguo na viatu duniani. Deportivo haifanyi makubwa sana kwenye soka, lakini mmiliki wake ana pesa balaa. 

Sheikh Mansour (Falme za Kiarabu)
 Utajiri: Dola bil 31.5 (tri 69)
 Klabu: Man City (England)
 Ni Mwarabu mwenye fedha chafu. Forbes mara nyingi imekuwa ikishindwa kumuweka miongoni mwa wamiliki matajiri zaidi, kwa kuwa utajiri wake ni wa familia, yaani wa kurithi. Hakuutafuta mwenyewe.Ni kijana mwenye miaka 44 ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa Falme za Kiarabu na memba wa familia ya kifalme ya Abu Dhabi. Jina lake kamili ni Mansour bin Zayed Al Nahyan. Anaongoza makampuni kibao ya migodi ya mafuta. 

George Soros (Marekani)
 Utajiri: Dola bil 19.2 (tri 42)
 Klabu: Manchester United (England)
 Bilionea huyu, 84, ana hisa za asilimia 7.85 katika Klabu ya Manchester United. Ana kampuni kubwa ya Solos Fund Management ambaye inahusiana na biashara zote zinazohusu fedha kama vile kubadilisha fedha na kusafirisha. Pia inasafirisha bidhaa kama madini, raba na kadhalika. 

Alisher Usmanov (Urusi)
 Utajiri: Dola bil 17.6 (tri 38.4)
 Klabu: Arsenal
 Ni Mrusi tajiri zaidi duniani. Ana hisa kadhaa katika Klabu ya Arsenal. Utajiri wake unatokana na biashara ya bidhaa zote za vyuma na madini akiwa na makampuni makubwa yanayoratibu biashara zake. 

Lakshmi Mittal (India)
 Utajiri: Dola bil 16.5 (tri 36)
 Klabu: QPR (England)
 Mhindi huyu bilionea anaishi jijini London na huko amekuwa akimwaga fedha balaa na ndiye mmiliki wa Klabu ya QPR ambayo msimu uliopita ilishuka daraja kutoka Ligi Kuu England. Ana asilimia 33 za hisa katika klabu hiyo.
 Kiwanda chake cha kutengeneza nondo ndiyo kikubwa zaidi duniani na ndicho kinachomuingizia fedha. 

Rinat Akhmetov (Ukraine)
 Utajiri: Dola bil 15.4 (tri 33.6)
 Klabu: Shakhtar Donetsk (Ukraine)
 Ni tajiri zaidi nchini Ukraine. Akhmetov ni mmiliki na rais wa Shakhtar Donetsk ambayo imetwaa ubingwa wa nchi hiyo mara saba ndani ya miaka 13. Ni mmiliki wa kampuni kubwa ya System Capital Management inayojihusisha na masuala ya kuuza madini, vyuma, mambo ya benki, bima, mawasiliano na vyombo vya habari. 

François Pinault (Ufaransa)
 Utajiri: Dola bil 15 (tri 33)
 Klabu: Rennes (Ufaransa)
 Anamiliki kampuni kubwa ya Karing ya Ufaransa ambayo inajihusisha na kuuza bidhaa mbalimbali zenye majina makubwa duniani kama pafyumu, nguo, vifaa vya michezo na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Rennes ya Ufaransa. 

Paul Allen (Marekani)
 Utajiri: Dola bil 15 (tri 33)
 Klabu: Seattle Sounders (Marekani)
 Alianzisha Kampuni ya Microsoft akiwa na Bill Gates. Anamiliki Klabu ya Seattle Sounders inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani. Utajiri wake unatokana na Kampuni ya Microsoft ambayo inahusika kusambaza ishu zote zinazohusu kompyuta duniani. 

Roman Abramovich (Urusi)
 Utajiri: Dola bil 10.2 (tri 22.3)
 Klabu: Chelsea
 Abramovich aliinunua Chelsea mwaka 2003 kwa dola milioni 233. Ndani ya miaka 10, bilionea huyu alikuwa ametumia dola bilioni 2.97 kwa ajili ya kikosi hicho. Ana Kampuni ya Millhouse Capital ambayo imewekeza kwenye mambo kibao ukiwemo usafiri wa anga, uchimbaji wa mafuta, umeme, bima na benki. 

Philip Anschutz (Marekani)
 Utajiri: Dola bil 10 (tri 21.8)
 Klabu: Los Angeles Galaxy (Marekani)
 Anschutz ametengeneza fedha kupitia mafuta, barabara za reli na mawasiliano. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Los Angeles Galaxy.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini