AJALI MBAYA YA GARI LA ABIRIA YATOKEA MOSHI

Hii ndiyo Hiace inavyoonekana mara baada ya kupata ajali

Wananchi wakienda kushuhudia ajali hiyo na kutoa msaada kwa majeruhi.
Wananchi wakiangalia Hiace hiyo iliyopata ajaliMajeruhi wa ajali hiyo wakiwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidiWananchi wakiuangalia mwili wa aliyefariki katika ajali hiyo (uliofunikwa kwa kitenge katikati ya barabara)Ajali mbaya ya gari imetokea hii leo katika eneo la KNCU barabara ya Kibosho Kirima Moshi Kilimanjaro, baada ya gari la abiria (hiace) kupata ajali huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi
Kwa mujibu wa ripota wa eddy blog aliyefika eneo hilo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni na abiria kadhaa wamejeruhiwa na kukumbizwa hospitali kwa matibabu zaidi huku abiria mmoja akihisiwa kufariki dunia katika ajali hiyo
Hizi ni taarifa za awali na eddy blog inaendelea kufuatilia taarifa za ajali hiyo ili uzipate kwa uhakika, endelea kuwa nasi mara mara
Picha na Thade Expensive wa eddy blog, Moshi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini