Wadada ambao mna sura nzuri, elimu nzuri, na hela kwani nini hamuoleki?
Jana nimekaa kijiweni na vijana wangu fulani, mida ya jioni jioni hivi, nikaanza kuwauliza kwa nini hawaoi. Sasa kila mtu na jibu lake, km vile: Bado najipanga, ndoa noma, mpaka nifikishe sijui miaka 30+, etc., Baadaye wakaanza kuwaongelea wadada wa kitaa na kusakiziana kuoa, wakiambiana kama vile, unasubiri nini, si umvute lara 1, mbona mdada yuko vizuri na kakamilika kila idara, mara mkuu yule demu mtoto wa nanii kaolewa? Vuta kifaa hicho, mbona kama mna ukaribu kiaina, mara yule dada huwa anapita na Prado mayai, badiebey vipi mkuu! Kula kichwa, n.k.
Cha ajabu sababu za vijana kutokuoa hazikuwa na mashiko hata kidogo! Mara baadaye wakajadili mademu karibu mtaa mzima na kuwataja watu wanaowachukua. Ndio jana nikakubali vijana mtaani wana databae kwenye vichwa vyao. "Bro huyo mbona demu, wa The Bossmkurugenzi wa ...., halafu yule mdingi mke wake anaishi Makongo juu, mara nyingi sana anakuja kushinda kwa demu wake, na hiyo nyumba kamjengea. Mara yule demu gari yake kanunuliwa na nani! Baadaye wakaconclude kwa kusema kwamba, bro, mademu wengi hapa mjini ni majanga, hasa wale wazuri na wenye elimu, na wenye vihela vya kuonekana wanaliwa sana. Nikawatajia kadhaa na kuwaambia mbona akina fulani, wana heshima sana na ni wanawake wazuri, wakaniambia bro we tatizo lako unashinda ofisini tuulize sisi huku kitaa!
Hii hali ya wadada wazuri na wenye elimu kutokuoleka chanzo chake hasa ni nini? Wadada wazuri na ambao mmesoma na kwa kiasi fulani wenye vihela ni kama vile vijana wanawakimbia na kudai nyie mlio wengi ni nyumba ndogo za wazee, hii ni kweli au uzushi? Kama ni kweli, siri ya ninyi kuwa small houses ni nini?
Siri ya ninyi kutokuoleka ni nini hasa?
Swali kwa wote: Ni kweli kwamba wadada wazuri na hasa wenye elimu ndio wanaoongoza kuteka wazee na kuwafanya wengi wa hao wazee kujisahau na hata kutelekeza wake na familia zao? Cha ajabu wadada wazuri hawazai lakini wanahisiwa kuwa na attachment kibao; je, wanaongoza kutoa mimba na kutumia vidonge vya kuzuia mimba? Ni kweli kwamba wadada wa mjini wazuri na wenye elimu wengi wao kuzaa ni mbinde pindi atakapoolewa?
Je, nini kifanyike kurekebisha hii hali?
Usiniulize wadada wazuri ndio wepi, jana vijana wangu waliniambia bro kuna mademu wakali hata kama uzuri hauna definition!