HATARI....POLISI YAKAMATA MABOMU MANNE YA KIVITA HUKO ZANZIBAR

Jeshi la polisi
Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu
manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu
yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali
mbali nchini.
Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame
amethibitisha kukamtwa kwa mtu huyo ambaye kwa Mujibu wa
jeshi hilo mtu huyo amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa
kuagiza, kuingiza na kuhifadhi mabomu ya kivita ya kurushwa
kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi
wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani
huku kamishna akidai mtandao huo unausishwa na matukio
kadhaa.
Hata hivyo kamishna Hamdani Maka amesema kukamtwa kwa
mtuhumiwa huyo ambaye hata hivyo amekataa kumtaja jina na
mazingira ya ukamataji wake amesema hausiani na imani ya kidini
na polisi inamshughulikia mtu kisheria kutokana na kosa lake
kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo Imani za kidini.
Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yeyote kuhusu mtuhumiwa
huyo jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo
mtu akipelekwa nje ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema
bado polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la
Zanzibar au la, ama ni mtandao wa ugaidi wa nchi nzima.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini