JAMAA ALIYEKUWA AKIWABAKA VIKONGWE ATIWA MBARONI HUKO KISARAWE PWANI

JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu (Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na wanawake na kutokomea kusikojulikana.





Alisema, William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.

Pia kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.


“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni maarufu kwa matukio ya ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa kunasua mitego aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu waandishi ili mumuone ni mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.


William alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa miaka ya hivi karibuni aliwahi kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha kosa ambalo lilimsababishia kuhukumiwa miaka 30 jela
Matei alisema kabla kifungo hicho hakijamalizika mwaka 2011 na 2012, William alikata rufaa na kutolewa ili kuendelea na taratibu nyingine na tangu hapo hakuonekana hadi polisi walipofanikiwa kumkamata kwa kosa la wizi wa mifugo.


Hata hivyo William alikana kuhusika na tuhuma zinazomkabili na kudai yeye sio Michael dada kama anavyoitwa bali ni Michael William na tuhuma za ubakaji ni za kusingiziwa.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini