AliKiba akanusha tetesi za kuwalipa waliomzomea Diamond Platnumz katika tamasha la Fiesta 2014 Dar es Salaam


Mkali wa jukwaa nchini, Ali Kiba amefunguka na kukanusha madai yaliyozuka mtaani baada ya kuzomewa kwa msanii mwenzake Diamond wakati wa tamasha la Fiesta 2014 kuwa alihusika kwa kuwalipa watu hao waliozomea.

Kiba amesema kuwa hata hajui uvumi huo umeanzia wapi na vipi kwani hawezi kufanya kitu kama hicho, hivyo hakuna ukweli wowote juu ya tetesi hizo ila kikubwa anawashukuru wana Dar es Salaam kwa mapokezi yao kwake kwani hakutegemea na amefurahishwa sana na imemtia moyo wa kuongeza bidii na kuandaa vitu vingine vikali zaidi.



Katika hatua nyingine Kiba amesema kuwa video ya ‘Mwana’ inatarajiwa kutoka muda wowote kati ya wiki hii au ijayo kwani ipo kwa ajili ya suprise yaa mashabiki wake wa kweli na wale wote wanaosapoti muziki wake.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini