China kufuta hukumu ya kifo?
Bunge
la China limeazimia kuondoa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa ambapo
rasimu ya mapendekezo ya marekebisho ya katiba tayari imewasilishwa
katika bunge la nchi hiyo.
Rasimu
ya mabadiliko hayo imewasilishwa kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya
kwanza katika kikao cha bunge hilo ambacho kinatarajiwa kukaa kwa muda
wa miezi 2.
Katika
mapendekezo hayo, makosa ambayo yametakiwa kuondolewa adhabu ya hukumu
ya kifo ni pamoja na kosa la usafirishaji ama kumiliki silaha na nyuklia
kinyume cha sheria, fedha badhia, kujipatia pesa kwa njia ya
udanganyifu, kujishughulisha na biashara ya ukahaba, kumzuia askari au
mwanajeshi kutimiza wajibu wake, na kuzusha uvumi wa uongo wakati wa
kupigana vita.
Iwapo
mabadiliko hayo yakifanyika, wale ambao wamekwishahukumiwa adhabu hiyo,
watabadilishiwa hukumu na badala yake kukabiliwa na kifungo cha muda
mrefu zaidi.
China
inatajwa kuwa ni moja ya nchi zinazoongoza kutoa hukumu ya kifo, ambapo
taasisi moja ya haki za binadamu ya Dui Hua imesema kwa mwaka jana peke
yake China imehukumu kifo kwa takribani watu 2,400 huku kukiwa hakuna
takwimu rasmi zilizopatikana mpaka sasa juu ya idadi ya watu
wanaonyongwa kila mwaka nchini humo.
Millardayo