UNYAMA! WAZAZI SOMENI HABARI HII YA KUSIKITISHA HAUSIGELI ALIVYOMFANYIA MTOTO

Na Imelda mtema
Unyama! Dada wa kazi (hausigeli), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi nyumba ya jirani.


Mtoto, Samwel John akiwa na maumivu makali aliyoyapata baada ya kujeruhiwa kwa kisu.

Akizungumzia mkasa huo kwa masikitiko makubwa uliojiri hivi karibuni maeneo hayo, baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la John alisema kuwa, siku ya tukio hilo alimuona hausigeli huyo akiwa amemshika mkono mwanaye huku akiwa na majeraha kwenye jicho na kichwani.
Alisema alipomuuliza nini kimetokea, hausigeli huyo alimjibu kuwa mtoto Samwel aligongwa na pikipiki.
John alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa kazi.




Baadhi ya majeraha ya kichwani aliyoyapata mtoto John.

“Nilikuwa nashangaa maana kila hausigeli huyo akizungumza kuwa mtoto amegongwa na pikipiki, mwanangu alikuwa akimnyooshea kidole na kusema kuwa yeye ndiye amemuumiza,” alisema mzazi huyo.
Mzazi huyo aliendelea kusema kwamba, baada ya kuona hivyo alimshika mkono mwanaye hadi kwenye nyumba ambayo anafanya kazi msichana huyo huku mtoto huyo akimuongoza chooni ambapo alikuta damu nyingi zimetapakaa.
Alisema kuwa alipoona hivyo ilibidi amchukue mwanaye na msichana huyo hadi polisi kwa ajili ya kupata PF-3 kwa ajili ya matibabu.Kwa upande wake hausigeli alipoulizwa ni kwa nini alifanya kitendo cha kinyama kiasi hicho alisema kuwa alikuwa akitamani kumtoa jicho mtoto huyo.



Wananchi wakishangaa unyama alioufanya hausigeli huyo.

“Alisema kuna shetani au roho ilikuwa ikimtuma amng’oe macho mwanangu,” alisema baba huyo.
Baada ya kujieleza, hausigeli huyo alitupwa korokoroni nyuma ya nondo za mahabusu kwa kitendo alichokifanya ambapo hadi gazeti hili linaanua jamvi maeneo hayo alikuwa kwenye Kituo cha Polisi cha Tabata akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini