NDUGU WAWILI WAUAWA KWA KUNYONGWA NA WATU WASIOJULIKANA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya
Watu wasiojulikana wamewanyonga hadi kufa ndugu wawili wakazi
wa maeneo ya Mtaa wa Madafu, Tandika jijini hapa.
Ndugu hao, Mwakamu Mariamu Buruhani (39) na Nuru Tumwanga
(42) walinyongwa usiku wa kuamkia jana.
Kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata, Mwakamu ni
mmiliki wa saluni iliyopo mtaa huo na inayoitwa Hair dressing.
Mmoja wa wafanyakazi wa saluni hiyo alidokeza kuwa, baada ya
kuona muda wa kufungua umepita, alimtuma kijana kwenda
kumwangalia Mwakamu na kumhimiza aje wafungue saluni hiyo.
Mfanyakazi huyo alisema kijana huyo alipofika alikuta mlango uko
wazi na Nuru alikuwa kitandani na mwenzake sakafuni sebuleni na
ndipo alipokwenda kumwita mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa
wa Mji Mpya, Wadadi Mtangwa na kisha kutoa taarifa polisi.
Polisi walifika na kuichukua miili hiyo na kuipeleka Hospitali ya
Temeke na uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wamenyongwa kwa
kuwa walikuwa na michubuko shingoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya, alikiri
kutokea tukio hilo.
Credits:Mwananchi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini