MLEGEZO WAMPONZA CHID BENZ ATAITIWA MAHAKAMANI, POLISI WATOKA NAYE MKUKU

KIBANO! Kuonesha wapo ‘serious’ na mavazi, polisi walimtaiti staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na kumtaka akavae vizuri kisha arejee mahakamani. Tukio hilo lilitokea juzi, Jumanne katika Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka yake ya kukutwa na madawa ya kulevya.

Staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa chini ya ulinzi mkali ndani ya Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Akiwa katika viunga hivyo vya mahakama, Chid Benz alionekana akiwa ametinga jinzi ambayo ililegezwa mkanda na alipoingia ndani ya chumba cha mahakama, mlegezo uliongezeka zaidi hadi kufikia chini ya makalio kitendo ambacho polisi walishindwa kukivumilia. Kuonesha kwamba hawakufurahishwa na kitendo hicho, maafande waliokuwa wakimsindikiza Chid mahakamani hapo, walimtaiti kwa kumshika kiunoni na kumtoa nje kwenda kumpandisha suruali hiyo kisha kumrudisha akiwa amevaa vizuri.
Mwana Hip hop huyo, ‘Chid Benz’ akivaa kwa adabu zaidi.
Akiwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Waliarwande Lema na mwendesha mashtaka, PP Mwanaamina Komba, Chid alisomewa mashtaka matatu alyokutwa nayo Oktoba 24, mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar. Mashtaka hayo ni; kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin gramu 0.25 yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi gramu 1.72 ambayo thamani yake ni Sh. 1,720 na vifaa vya kuvutia (kifuu cha nazi na kijiko).


Chid aliyakana mashtaka yote matatu hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu na kuweka dhamana wazi ya faini ya shilingi milioni moja na wadhamini wawili lakini mshtakiwa hakukidhi masharti ya dhamana, akaomba kukamilisha masharti hayo kesho yake (Jumatano) hivyo akarudishwa mahabusu Segerea.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini