BINTI ATEKWA NA WACHUNA NGOZI
Binti anayetambulika kwa jina la Latifa Abdallah
(wa pili kushoto) akiwa na ndugu zake
|
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
MBONA majanga!
Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Latifa Abdallah (19), mkazi wa
Kinondoni –Mkwajuni, Dar amesimulia alivyotekwa na watu aliodai ni
wachuna ngozi wakiwa na mwanamke aliyevalia kininja ndani ya gari jeusi.
Akizungumza na
Uwazi jijini Dar, juzi, Latifa alidai Oktoba 19, mwaka huu akiwa anatoka
kumsindikiza dada yake aliyekuwa akienda Kibaha, Pwani ghafla msichana
aliyevalia kininja akajigonga kwenye mwamvuli alioushika na kumwambia
alimgonga kwa makusudi.
“Nilimwomba
msamaha na kumwambia ni bahati mbaya lakini alinikamata na kuniingiza
ndani ya gari jeusi lililopaki kando ya barabara ambapo kuna mtu
alifungua mlango yule mwanamke akanisukumia ndani,” alisema Latifa.
Akizidi
kusimulia, binti huyo alisema kuwa, ndani ya gari hilo alimkuta msichana
mmoja kama yeye na mtoto kama wa miaka miwili wakiwa wamefungwa
vitambaa vyeusi machoni na yeye akafungwa kama wenzake.
“Tulikwenda
kushushwa kwenye nyumba moja sijui ni wapi, tukaingizwa katika chumba
kidogo na kufunguliwa vitambaa. Ndipo nilipogundua kuwa, watekaji wote
walivaa kininja. Mmoja alikuwa mwanaume, mwingine ndiyo yule
aliyenisukumia ndani ya gari pale kwenye Kituo cha Daladala cha Vijana
Kinondoni (Dar).
Fomu ya PF3 ya Latifa Abdalla aliyopewa kituo cha Polisi Oysterbay.
“Yule mwanaume
alisema lazima tufanye naye mapenzi la sivyo atatufanya kama
watakavyomfanyia yule mtoto. Wakamchukua yule mtoto na kumchoma sindano,
alilia sana kisha akanyamza ghafla huku ngozi yake ikiumuka kama puto.
Yule mwanaume alitoa kisu na kuanza kumchuna ngozi yule mtoto akianzia
shingoni.
“Nikiwa katika
hali ya kutetemeka kwa woga, yule mwanamke alisema tujiandae na kifo
kama cha yule mtoto. Nilimwomba Mungu sana atuepushie kifo hicho.
“Siku ya
Jumanne asubuhi wale watu walikuja kutuangalia kidogo na kuondoka.
Baadaye jioni walirudi na kutupa maji ambayo hatukuelewa ndani yake
yalikuwa na nini, walitunywesha na kutuambia kesho yake wangeturudisha
makwetu, wakachukua namba za simu za ndugu zetu, sikuamini nikawatajia
namba ya mwalimu wangu wa cherehani ambaye waliniambia akipokea
nimwambie kuwa mimi ni mzima nitafika nyumbani kesho kutokea Kawe jambo
ambalo nililifanya.
“Kuanzia hapo
yule mwanamke akawa anachati naye. Wakati huo yule mwenzangu kwao ni
Mbezi naye aliwataarifu ndugu zake na tukawa tunasubiri kesho ifike.
Kweli, kesho yake wakatuchukua, mimi nikashushwa pale Kituo cha Daladala
Kinondoni–Studio (Dar), wakanipa shilingi 1,000 wakasema nipande
bodaboda nirudi nyumbani,” alisema Latifa.
Mwalimu wa
cherehani wa Latifa, Celestine ‘Baba Mkanji’ alisema tangu Latifa
atoweke nyumbani amekuwa akipigiwa simu na kutumiwa meseji zinazoonesha
Latifa alikuwa kwenye hali ya hatari jambo lililomshtua na
kuwashirikisha ndugu zake nao wakaripoti Kituo cha Polisi cha
Mzambarauni, baadaye Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar.
Baada
ya kurudishwa nyumbani, Latifa alipelekwa Oysterbay Polisi kwa ajili ya
kupata PF3 na baadaye kwenda Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya
vipimo zaidi.
Naye mama mzazi wa
Latifa, Habiba Saidi (56) alisema amesikitishwa na kitendo
alichofanyiwa mwanaye na kuomba watu wa haki za binadamu na wanasheria
wamsaidie ili waliomfanyia mambo hayo mwanaye wakamatwe.