Je, Umesikia story ya uwanja wa ndege kupata tatizo la IT? Isome hapa.
Imetokea mara nyingi kusikia Watanzania wakilalamika
masuala mbali mbali, mfano ni huu. Unakumbuka ni mara
ngapi unahitaji kutoa pesa ATM na ukakuta haiifanyi kazi
kutokana na tatizo la Network? Au unakumbuka ni mara ngapi
unapiga simu halafu unajibiwa namba haipatikani?
Sasa story ni kwamba hayo mambo ya ‘system failure’ au
matatizo ya mtandao hata Ulaya yapo, headline kutoka
Uingereza inasema wafanyakazi katika uwanja wa ndege
ambao uko busy zaidi Uingereza wa Heathrow, walijikuta na
jukumu la kubeba mizigo ya abiria kwa mikono kutokana na
mfumo wa IT kusumbua kwa takribani saa 1 uwanjani hapo.
Usumbufu uliojitokeza umepelekea pia tatizo la ratiba za ndege
mtandaoni kuvurugika, japo mamlaka za uwanja huo ziliarifu
kulimaliza tatizo hilo na kila kitu kuendelea kama ilivyo
kawaida.