MAUAJI YA KUTISHA LUDEWA NJOMBE, ATANDIKWA NONDO KICHWANI HADI AKAFA

 Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio


 majirani wakiuangaliwa mwili wa marehemu Mgimba.
Mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina la Merkion Mgimba(Msuruisi) miaka 70 mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ameuawa kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28 oktoba 2014 akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga alisema kuwa marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la kujisaidia haja ndogo lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake na kuanza kupambana naye ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani akipiga kelele.

Bi.Theodora alisema baada ya kusikia kelele hizo sebuleni alilazimika kutoka chumbani ili aende kutoa msaada kwa mume wake lakini alipofungua mlango wachumbani alikutana na nondo iliyompata mkononi ndipo alipofanya uamuzi wa kutokea dirishani ili aende kuomba msaada lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwani alishuhudia mtu aliyevalia shati jeupe akitokomea gizani.

Alisema baada ya muuaji huyo kukimbia alirudi kuona hali ya mumewe lakini alimkuta tayari ameshaaga Dunia,hapo akachukua uamuzi wa kwenda kuwaeleza majirani na kiongozi wa mtaa ili kumsaka muuaji huyo ambaye hakuweza kumfahamu zaidi ya kushuhudia shati lake jeupe.

“Nilisikia mumewangu akikimbia kutoka nje na baadae kelele sebuleni ndipo nilipotoka ili kutoa msaada lakini nilipofungua mlango wa chumbani muuaji huyo alinipiga na nondo mkononi ikanilazimu kufunga mlango na kurudi chumbani nikisikia mume wangu akilia kwa uchungu,nikaamua kupitia dirishani ili niombe msaada kwa majirani ndipo nilipomuona muuaji huyo akikimbia kichakani”,Alisema Bi.Theodora.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini