DARASA LA MAPENZI:HIZI NDIZO NJIA ZA KUMTAMBUA MWANAMKE WAKO KUWA ANAKUPENDA AU ANAKUTUMIA!!





Zipo nyingi sana, lakini hapa nitakupa dalili ambazo ukiona mwanamke wako anazo ujue hana penzi la moyoni.

ANAKUTEKA
Mwanamke ana haki ya kudeka kwa mwanaume wake, lakini siyo kwa nia nyingine yoyote zaidi ya kunakshi penzi. Huyu hana nia hiyo, anadeka kwa ajili ya kukupagawisha kimahaba ili aweze kuzishika hisia zako sawasawa.
Mchunguze vizuri, utagundua kwamba hata sauti yake anayoitumia kuzungumza na wewe siyo anayotumia akiwa na shoga zake. Anailegeza kwa kuiremba kwa kila hali.
Anataka kukupagawisha. Hiyo ndiyo nia yake, kukupagawisha sana maana yake hutapindua na hutakuwa na wazo la kuwa na mtu mwingine zaidi yake.


ANAPENDA FEDHA
Ni kawaida mwanamke kumuomba fedha mpenzi wake, lakini huyu asiye na mapenzi ya kweli, huwaza fedha mara zote.
Hata kama utazungumza kuhusu kutoka naye katika matembezi, bado ataulizia kuhusu dau lake.
Ana mahitaji mengi. Mwanamke wa aina hii, ukitoka naye nje ya mji au kulala naye hotelini, asubuhi atataka chake! Jiulize ni mpenzi wako au anajiuza? Mbaya zaidi, hata kama utakuwa mgonjwa na amekuja kukutazama siyo ajabu kabisa kukuomba fedha, akiwa na tabia hii ujue hana mapenzi, anataka kukutumia.

HANA HESHIMA


Kwa kuwa hakupendi na wala hafikirii kuwa na wewe katika ndoa, sifa za uanamke hatakuwa nazo. Inawezekana kabisa anazifahamu vizuri sana sifa hizo, lakini hana muda nazo.
Hasikii ukimwambia kitu, mjeuri na wala haheshimu kauli zako.
Kama mpenzi wako, ambaye una malengo naye ya baadaye, una haki ya kumzuia aina fulani ya mavazi, kampani au tabia ambazo huzipendi.
Kwa mwanamke wa aina hii, kumwambia ni sawa na kumruhusu! Mwanamke huyu, neno heshima ni msamiati mgumu sana kwake.
Unajua kwa nini? Kwa sababu hakupendi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini