UNAKUMBUKA WALE WASICHANA 200 WALIOTEKWA NA BOKO HARAM? MMOJA AMETOROKA NA KUSIMULIA HALI ILIVYO

Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la
Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini
mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka
wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya
BBC.
Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika
makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua
itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi
hilo .
'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu
aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama
utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na
kuacha maiti yangu ikusachukuliwa nilikuwa nalia na kuomba
mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka
mikononi mwa Boko Haram
Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya
BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori
wakati wanapinaji wa Boko Haramu walipomteka yeye na
wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana 200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa
lakini wale waliokimbia walibahatika kutoingia katika hofu kubwa
kwenye mikono ya watekaji.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights
Watch limesema wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko
Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa na hata
kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa
Kiislam wamewawateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana
tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya
kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram ambayo hatua
itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru wasichana wa hao
waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano
yoyote ya kusitisha mapigano na hakuna dalili zozote za kuachiwa
kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia
bado yanawasumbua..
bbc

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …