Baada ya Tatoo ya Jina, Nuhu Mziwanda achora tatoo yenye sura ya Shilole

Mambo ya Mahaba nipeleke West Africa nikateketee kwa Ebola yule Mpenzi wa Shilole Nuhu Mziwanda ameamua kuchora tatoo mkononi yenye sura ya Shilole kuonesha mapenzi yake kwa bidada.

Hii imekuja siku chache baada ya Shilole kuwashukia wanaomsema vibaya mpenzi wake kuwa ni mtoto, anambembenda kwasababu wapo kama mtu na mwanae,mara kijana anapenda kulelewa.Ndio Shilole alijibu kuwa huyo si mtoto kwani mapenzi anayompa chumbani ni mazito na angekuwa mtoto asingekuwa analilia mapenzi bali angekuwa analilia nyonyo kwa mama ake.

Baada siku kadhaa ndio kijana huyo akaibuka na tatoo ya hiyo kudhihirisha mapenzi kwa mwanadafada huyo. Hii ni tatoo ya pili Nuhu kujichora baada ya ile ya kwanza yenye jina la ShishiBaby. 

Btw hatuombei waachane ila siku wakiachana sijui itakuwaje?

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini