Kilichowakuta CHADEMA walioandamana Mwanza Sept.25

Kutoka 88.1 Mwanza ambapo Polisi wamekamata viongozi sita na wafuasi kadhaa wa (CHADEMA) waliokuwa wakijiandaa kuandamana baada ya kukaidi amri ya polisi kusitisha maandamano.
Ni September 25 saa 5.40 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kwa maandamano yaliyokuwa yaanzie viwanja vya Sahara mpaka ofisi za mkuu wa wilaya ya Nyamagana na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe.
Purukushani ilidumu kwa zaidi ya dakika 120 ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu huku taarifa zisizo rasmi zikisema Polisi wamewatia mbaroni watu 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.



Kwa mujibu wa ripota wa nguvu Albert G. Sengo, licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili ambapo John Nzwalile katibu wa CHADEMA Mwanza amesema >>> ‘naweza kusema kwa ujumla tumefanikiwa, Polisi ndio wameandamana kwa wingi kuliko hata sisi, tokea asubuhi ukienda chooni au kunywa chai Askari kanzu wanakufatili, ukinywa chai na wao wanajifanya wanakunywa chai
 ‘Niseme maandamano yetu yamefanikiwa kwa sababu yalikua yamepangwa kwa akili kubwa sana, tuliandamana kuanzia kichwani… hatukuandamana ovyoovyo, hawakujua tunaanzia wapi tunaishia wapi…. tumeshangaa Polisi wamekuja na vifaa utadhani unaangalia movie ya vita’
‘Mpaka sasa taarifa nilizonazo mwenyekiti wangu wa Nyamagana amekamatwa, Katibu mwenezi Nyamagana, Mwenyekiti kata ya Bugogwa, Katibu wilaya ya Ilemela wamekamatwa…. watu ambao kosa lao ni kuwaambia Watanzania kuna pesa inaliwa na Wabunge kwenye batili la katiba’
‘Kwa kauli moja ya chama niseme tu kwamba maandamano na migomo isiyokua na kikomo itaendelea…. tunazidi kujipanga vizuri kuangalia namna bora zaidi ya kuandamana, tunataka watu wetu watoke Wanasheria wetu wanajipanga…. kuhakikisha wanatoka bila masharti’

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini