MAELFU YA WATANZANIA WAENDELEA KUFA KATIKA AJALI ZA BARABARANI


Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu elfu thelathini na moja, mia tatu na kumi na tatu wamefariki dunia kutokana na ajali za barabarani zilizotokea kati ya 2005 hadi sasa.
Vifo hivyo vimetokana na ajali laki moja, elfu tisini na tisa na mia sita arobaini na nane ambapo jumla ya watu laki moja na elfu sabini na tano, mia moja sabini na tano wamejeruhiwa.


Mwaka mbaya kuliko yote kwa mujibu wa takwimu hizo ni mwaka 2013 ambapo jumla ya watu 4002 walifariki kutokana na ajali za barabarani, huku wengine 20,689 wakipata majeraha katika sehemu mbali mbali za miili yao.

Hata hivyo mwaka huu huenda hali ikawa tofauti kwani kati ya Januari na sasa watu waliofariki kwa ajali ni 1743 katika ajali 8405 huku waliojeruhiwa wakiwa ni watu elfu saba.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini