WEMA ATOSWA VIKAO VYA HARUSI YA DIAMOND





Meninah
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media nyinmgine kuziandika kwa kasi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini