UGONJWA WA EBOLA NA JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NAO. PIX 1

PIX 1Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akisalimiana na Wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa  abiria  atayekutwa na ugonjwa wa Ebola  mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam..

PIX 2Baadhi ya Wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa Wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola iliyoko katika eneo la Hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam.
PIX 3Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili toka kushoto) akiwaangalia Wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa Ebola wakati alipokagua Wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola iliyoko katika eneo la Hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam.
UGONJWA WA EBOLA NA JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NAO.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
22/09/2014.
Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya homa ya hemorajiikimaanisha ugonjwa wa kumwagika damu bila kuganda (Viral Haemorrhagic Fevers).
 Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, ugonjwa huu ni hatari na unasababishwa na kirusi kiitwacho ebola kwani kirusi hicho ni moja kati ya familia ya virusi watatu toka katika familia yafiloviridiae.
 Kuna aina tano za kirusi cha ebola ambao ni bundibugyo ebolavirus(BDBV), Zaire Ebolavirus (EBOV), Reston Ebolavirus (RESTV), Sudan Ebolavirus (SUDV) na Tai Forest Ebolavirus (TAFV).
 Ni ugongwa unaoua kwa kasi na tafiti zinaonyesha kwamba katika orodha ya watu 10 walioambukizwa na virusi vya ugonjwa huo, basi wastani kati ya watano au tisa hufariki.
 Aina hizo tatu za virusi, yaani BDBV, EBOV na RESTV, ndiyo inayongoza kwa kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo Barani Afrika wakati aina nyingine za virusi hao wanapatikana katika nchi za Asia, yaani Ufilipino na Thailand.
 Taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza ugonjwa huu uliripotiwa kutokea mnamo mwaka 1976 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na taarifa zinaeleza kuwa hatari ya mgojwa kupoteza maisha ni asilimia 90.
 Tafiti zinaonyesha kuwa, kuwa Popo wanaopenda kula matunda wanaeneza ugonjwa huo bila wao kuaathirika na katika jamii yetu ugonjwa huo huweza kuambukizwa kutoka mtu mmoja mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine baada ya kugusana na damu au maji maji kupitia michubuko au majeraha yaliyopo juu ya ngozi.
 Pia watu ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo ni jamii inayoishi karibu na jamii ya wanyama ambao mara nyingi ni Nyani, Sokwe, Tumbili pamoja na Popo.
 Licha ya watu walio na maambukizi ya ugonjwa huo kapata nafuu, lakini bado wanaweza kuwaambukiza wengine kwa njia mbalimbali, mfano kwa njia ya kujamiana.
 Wataalam wanaamini kuwa virusi vya ugonjwa huo huwa havienei kwa njia ya hewa bali kwa mtu kugusana na majimaji ya mwili, kama vile matapishi, mate, jasho, machozi, ama manii au shahawa ya mtu aliyeathirika na ugonjwa huo.
 Kwa upande mwingine hata Madaktari na wauguzi, wanaowatunza wagonjwa wa ebola, watu wenye uhusiano wa karibu na mtu aliyeambukizwa, watu wanaogusa maiti ya mtu mwenye virusi hivyo wapo katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ebola.
 Ishara na dalili muhimu ya ugonjwa huu ni hali ya kutokwa na damu katika sehemu tofauti za mwili kama vile katika ufizi, pua, katika njia ya haja, lakini kabla mgonjwa hajafikia daraja hilo, kwanza mtu huwa na homa kali, viwango vya joto vya mwili hupanda sana, kisha anaweza kuwa anajisikia kutapika, na hata kutapika kwenyewe, kuharisha, na pia kuwa mnyonge huku viungo vyake vikiwa na maumivu.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini